Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo February 8 2017
ametangaza kuiachia orodha ya Watu 65 wanaotuhumiwa kwa biashara ya dawa
za kulevya ambapo amemtaja pia Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe
ndani yake.
Dakika chache baada ya kumtaja, CHADEMA Makao makuu Dar es salaam
walikutana na Waandishi wa habari na kusema yafuatayo >>>
“Kimsingi katika majina mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa
chama Mbowe, swala la utetezi wake au maelezo hilo ni swala binafsi
sababu kilichotajwa ni jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii
kulaani“
“Tunalaani jinsi tusivyoweza kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi
yetu na jinsi tusivyofata kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria, Mh. Mbowe
ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni,
ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za kufata unapokua na kusudio
la kumuita“
‘Kitendo cha kwenda kuongea kwenye mkutano na Waandishi wa habari na
kutaja viongozi wakuu wa kitaifa ambao wana tuhuma tu ambazo
hazijathibitishwa, ni kukosa ustaarabu wa kiuongozi… tusingependa kuona
viongozi wengine Waandamizi kutendewa kama alivyotendewa kiongozi wa
chama chetu“
No comments:
Post a Comment