Wakati
Wizara ya Katiba na Sheria ikiingia rasmi katika ofisi zake mpya mjini
Dodoma jana baada ya kuhamia mwishoni mwa wiki, Wizara ya Kilimo, Mifugo
na Uvuvi nayo imetangaza kuhamia mjini humo wiki mbili zijazo, huku
ikiwatoa hofu watumishi wanaohamia huko kwa kuwataka kutekeleza majukumu
yao ipasavyo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Mathew Mtigumwe, amewatoa hofu
watumishi wa wizara yake kuwa suala la kuhamia Dodoma kuwa litafuata
misingi na stahili za watumishi kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa
umma.
Ameyasema
hayo wakati wa kikao maalumu kilicholenga kujadili kwa pamoja namna ya
utendaji kazi katika wizara hiyo sambamba na kutoa utaratibu
utakavyokuwa kuelekea kuhamia makao makuu ya nchi Dodoma.
Amesema
awamu ya kwanza ya uhamisho utahusisha watumishi 88 kutoka Idara Kuu ya
Mazao, watumishi 41 watahamia Dodoma kuanzia Februari 14 na 15, mwaka
huu huku wengine 47 watahamia muda wowote kati ya mwezi huu na Juni
mwaka huu.
Aidha,
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua rasmi
ofisi za wizara yake Dodoma na kuwataka watumishi waliohamia kutekeleza
majukumu yao ipasavyo.
Hilo
limekuja mara baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutoa mwelekeo wa
kuhamia makao makuu ya nchi kwa Mawaziri kwamba ifikapo Februari 28,
mwaka huu, tayari wizara kadhaa ziwe zimehamia Dodoma ikiwemo ya Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyohamia wiki
iliyopita.
No comments:
Post a Comment