Waziri wa Mambo ya Ndani, mheshimiwa Mwingulu Nchemba, amekilaani kitendo cha askari aliyemtishia bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye jana wakati akitaka kuzungumza na waandishi wa habari.
Mheshimiwa Mwigulu ameahidi kumsaka askari huyo ili sheria ifuate mkondo wake.
“Mh.Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu,” ameandika kwenye akaunti yake ya Instagram.
“Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini,” ameongeza.
“Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.”
Kabla ya kuanza kuzungumza na waandishi wa habari, Nape alizuiliwa na askari kadhaa walionekana kwenye video wakimlamzimisha arudi ndani ya gari lake kabla ya mmoja kuchomoa bastola.
“Kwanini mnatoa bunduki hadharani, mimi jambazi?” alihoji Nape.
“Nataka waliokuja kuzuia mkutano waambie kwanini wanazuia mkutano. Wanatoa bunduki hadharani, wanataka sasa nifanye nisivyowaza kufanya. They want to kill me. Nataka hawa waliotoa bunduki kwenye nchi huru waseme aliyewatuma kutoa bunduki hadharani, aliyetuma kuzuia mkutano, I want this kabla sijaingia kwenye gari kuondoka, tusifanyiane mambo ya kijinga nchi huru hii. Nimepigana mimi kutafuta kura za CCM halafu wanakuja wapuuzi wachache.”
No comments:
Post a Comment