Mohammed
Matumla amepigwa na kuumizwa vibaya hali iliyosababishwa akimbizwe
hospitali ya Temeke kwa kutumia gari dogo la mizigo au pick up.
Matumla ambaye ni mtoto wa bondia nyota wa zamani, Rashid Matumla amepigwa katika raundi ya saba na bondia Mfaume Mfaume.
Pambano lao lilikuwa la utangulizi lililokuwa likisubiriwa kwa hamu zaidi leo.
Matumla
alianza kupoteza mwelekeo katika raundi ya tano lakini akajitutumua
hadi raundi ya saba ambayo aliambulia kipigo kikali kutoka kwa Mfaume.
Baada
ya kusukumiwa ngumi mfululizo, alianguka lakini akaonekana ni kama mtu
aliyechanganyikiwa, akitaka kukimbia. wakamuhi na kumzuia na baadaye
kumlaza chini.
Daktari
aliyekuwa mtazamaji, ndiye alilazimika kumtibu kwa ajili ya huduma ya
kwanza kwa kuwa hakukuwa na huduma ya kwanza wala gari la wagonjwa
ukumbini hapo.
Wakati anaondolewa ukumbini hapo, hali yake haikuwa nzuri na alikimbizwa katika hospitali ya Temeke.
No comments:
Post a Comment