Friday, February 10, 2017

MBOWE: SIENDI POLISI KWA WITO WA MAKONDA

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe 
Dodoma. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema hatafika polisi kwa kuitwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo, Mbowe amesema yuko tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kama utaratibu wa kisheria utafuatwa.                    

“Makonda hana mamlaka ya kumpa wito mtu kwenda polisi kwa mujibu wa sheria ya serikali za mitaa,”amesema Mbowe.

“Makonda amemchafulia jina langu, chama, familia na upinzani.”     

No comments:

Post a Comment