Mbunge
wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Freeman Aikaeli Mbowe amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda hana mamlaka ya kumuita kwenda Kituo cha Polisi.
Mbowe
ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Mjini
Dodoma kufuatia kutajwa katika orodha ya watuhumiwa 65 wanaojihusisha na
biashara ya dawa za kulevya na kutakiwa kufika Kituo cha Polisi cha
Kati jijini Dar es Salaam leo saa tano asubuhi.
Mbowe
amekanusha vikali tuhuma hizo za kujihusisha na biashara ya dawa za
kulevya na kusema kuwa anachokifanya RC Makonda ni kuwaepusha watuhumiwa
wa kweli wa dawa za kulevya na mikononi mwa sheria.
Aidha, Mbowe amesema kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi muda wowote endapo njia sahihi zitakapofuatwa.
Pia amesema atamfungulia mashtaka RC Paul Makonda kwa kumchafulia jina lake kufuatia kumtuhumu kwa biashara ya dawa za kulevya.
Kiongozi huyo wa Kambi ya Upinzani Bungeni amesema kuwa wao hawana ugomvi wowote na Jamhuri bali Paul Makonda binafsi.
No comments:
Post a Comment