Ushindi
una raha yake na mastaa wa Simba hivi sasa wanatembea kifua mbele
kutokana na kufurahiwa na kila mdau wa timu hiyo lakini juzi walipewa
mamilioni ya tajiri Mohamed Dewji ‘Mo’ huku viongozi wengine wa klabu
hiyo nao wakiwamwagia mamilioni mengine.
Raha yote hiyo inatokana na kuifunga Yanga mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, juzi na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa tofauti ya pointi tano.
Habari
kutoka ndani ya Simba, zimedai kuwa, juzi Jumamosi kabla ya mchezo huo,
wachezaji hao walipewa Sh 5,000,000 kutoka kwa Mo wagawane lakini pia
wakaahidiwa Sh milioni 15 za papo kwa papo kama wataifunga Yanga.
Mmoja
wa viongozi wa timu hiyo ambaye aliomba kutotajwa jina lake alisema:
“Hali hiyo iliwafanya wachezaji wapambane vilivyo uwanjani na baada tu
ya mechi hiyo walipewa fedha zao hizo milioni 15 na kugawana.
“Lakini
pia leo hii kuna milioni 15 nyingine watapewa watakapokutana na uongozi
kwa lengo la kuwapongeza kutokana na kazi yao kubwa waliyoifanya
uwanjani jana (juzi) lakini pia kuna uwezekano pia mwanachama wetu
Mohamed Dewji naye akatoa kiasi kama hicho cha fedha kwani pia aliahidi
kuwashangaza wachezaji wetu kama wataifunga Yanga,” kilisema chanzo
hicho cha habari.
Katika
hatua nyingine kikosi hicho cha Simba leo hii asubuhi kitaendelea na
mazoezi yake ya kujiandaa na mechi zake za ligi kuu pamoja na Kombe la
FA zilizobakia.
Kocha
Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, amesema mazoezi hayo yatafanyika
katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment