Mshambuliaji nyota wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo, ameweka bayana kwamba, sasa ubingwa upo wazi kwa upande wao, baada ya kuwafunga wapinzani wao, Yanga na kufikisha gepu la pointi tano mbele yao, jambo ambalo linawafanya kuendelea kung’ang’ania kileleni.
Mavugo
alichangia kwa kiasi kikubwa ushindi wa Simba wa mabao 2-1 dhidi ya
Yanga kwenye mechi ya ligi kuu iliyopigwa Uwanja wa Taifa, Dar. Bao
lingine la Simba lilifungwa na Shiza Kichuya na Yanga wao walifunga
kupitia kwa Simon Msuva.
Mavugo
amesema kwamba njia ya ubingwa ipo wazi kwa kuwa Yanga ndiyo ilikuwa
timu pekee ambayo waliifikiria inaweza kuharibu mipango yao lakini baada
ya kuifunga hakuna ambaye anaweza kuwazuia tena.
“Hakuna
ambaye anaweza kutuzuia tena baada ya kuifunga Yanga kwa sababu wao
ndiyo walikuwa wapinzani wetu na ambao tulikuwa tukiwahofia kwamba
wanaweza kutuvurugia malengo yetu ya kuwapa ubingwa mashabiki ambao
wamekuwa wakiungojea kwa hamu.
“Kilichobaki
ni kushinda mechi hizi saba zilizobakia na tunajua hakuna ambaye
atatuzuia kushinda kwa sababu sisi ni bora na tuna muunganiko mzuri
ambao ndiyo unachangia kwa kiasi kikubwa kushinda mechi zetu,” alisema
Mavugo.
No comments:
Post a Comment