Uholanzi imemtimua kocha wa timu yake ya taifa Danny Blind baada ya kudumu kwa takriban miaka miwili.
Hii inafuatia kichapo cha magoli 2-0 dhidi ya Bulgaria siku ya Jumamosi
na kuwaacha Uholanzi katika nafasi ya nne kwenye mbio za kufuzu
kushiriki kombe la dunia.
Blind mwenye miaka 55 alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Guus Hiddink
mwaka 2015 huku ikishuhudiwa kikosi chake kikishindwa kufuzu fainali za
michuano ya Ulaya mwaka jana.
Chama cha soka nchini Uholanzi kimesema kuwa ameicha timu hiyo katika wakati mgumu kufuzu kucheza kombe la dunia nchini Urusi.
Fred Grim ameteuliwa kuwa kocha wa mpito na atakiongoza kikosi hicho siku ya Jumanne dhidi ya Ufaransa.
No comments:
Post a Comment