Askofu
mstaafu wa kanisa la Pentekoste (FPCT) Singida mjini Dk. Paul Samweli,
amesema suala la serikali ya Dk. John Magufuli kusisitiza ulipaji wa
kodi na ushuru ni utekelezaji wa maagizo ya Yesu Kristo, hivyo waumini
na Watanzania kwa ujumla, wanatakiwa kutii na kuzingatia wajibu wao huo.
Akiijengea
nguvu hoja yake hiyo, amesema kwa mujibu wa kitabu kitakatifu cha
Mungu cha biblia Warumi 13 (msitari 1-14), inaonesha wazi Yesu kristo
alipigia debe Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA).
Askofu
Paul alisema katika Warumi 13 kimeainisha kuwa watoza kodi na ushuru,
ni wahudumu wa Mungu kuwa wapeni haki zao, mtu wa kodi, kodi, mtu wa
ushuru, ushuru.
Dk.
Paul amesema hayo juzi wakati akihubiri kwenye ibada ya kawaida ambayo
pia ilihudhuriwa na kamanda wa jeshi la polisi mkoa mkoani hapa ACP
Debora Daudi Magiligimba.
Akisisitiza,
alisema kwa vile ulipaji kodi umepewa baraka zote na Mwenyezi Mungu,
waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini, wanapaswa kuwa mstari wa mbele
katika kutii agizo la Mungu la kulipa kodi uliowekwa kisheria bila
shurti.
“Serikali
ya Rais Magufuli katika hili la uhimizaji wa ulipaji kodi na ushuru,
inafanya vizuri kazi iliyopo mbele yetu waumini wa dini na Watanzania
kwa ujumla, ni kulipa kodi na ushuru kwa wakati, ili nchi yetu iweze
kusonga mbele kimaendeleo. Haya mambo ya kukwepa kulipa kodi au ushuru,
yakomeshwe,” alisema.
Kuhusu
watoza kodi na ushuru Dk.Paul, alisema kuwa katika Biblia (Luka
Mtakatifu 3 -12-17) inasema watoza kodi/ushuru waliagizwa wasitoze
kubwa ambayo itakuwa kinyume na sheria inavyoagiza.
Akifafanua,
alisema wafanyakazi wa TRA, katika utekelezaji wa majukumu yao,
wanatakiwa kutoza kodi na ushuru kwa mujibu na sheria, kanuni na
taratibu zilizowekwa na si vinginevyo.
“Wakitoza
kodi au ushuru mkubwa ambao upo kinyume na sheria, watakuwa
wanamudhulumu mlipaji, kitendo hicho sio tu binadamu mwenye maadili mema
hakipendi, lakini pia, nacho hakitampendeza Mwenyezi Mungu,” alisema.
Kwaupande
wa jeshi la polisi, Dk. Paul amesema kwamba katika kitabu cha Warumi 3
mstari wa 14, kimewataka askari polisi katika kutekeleza majukumu yao,
wasidhulumu mtu wala wasiwababikizie watu kesi za uongo. Pia watosheke
na mshahara wanaolipwa.
“Kamanda
maneno yaliyotamkwa na mtumishi wa Mungu Yohana, yanamtaka kila
askari polisi, aridhike na mshahara wake. Ina maana asiwe na tamaa ya
kuomba rushwa na vile vile asibabikie mwananchi kesi, bali atatekeleza
wajibu wake kwa mujibu wa mkataba wake wa kazi,” alisema.
Dk.
Paul alitumia fursa hiyo kulipongeza jeshi la polisi mkoa wa Singida
kwa juhudi zake za kudhibiti vitendo vya kihalifu ambavyo vinaweza
kuhatalisha amani na utulivu ulipo.
“Nikupongeze
kipekee kamanda Magiligimba kwa kuazisha utamaduni mpya wa kuongea na
waumini wa madhehebu ya dini kwenye nyumba zao ibada. Pia kwa uamuzi
wako wa kudhibiti uhalifu kabla haujatokea. Kwa kifupi unataka dalili za
kutokea uhalifu, zishughulikiwe mapema kabla hazijaleta madhara. Sisi
kanisa tunakuunga mkono katika hili. Mungu akutangulie,” alisema
Dk.Paul.
No comments:
Post a Comment