Serikali imesema haitamvumilia mtumishi wa umma mzembe ambaye anakaa ofisini badala ya kuwahudumia wananchi katika maeneo yao.
Hayo yamebainishwa na waziri wa maji na umwagiliaji , Profesa Makame Mbarawa, alipotembelea mradi wa maji Ngapa kuangalia maendeleo yake.
Aidha waziri Mbarawa akawataka pia wataalamu wa idara ya maji nchini kuwasimamaia wakandarasi ambao wamewapa kazi katika eneo husika ili miradi waliyopewa iweze kukamilika kwa wakati.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na majitaka mjini Lindi, LUWASA, Mhandisi Soud Juma, akazungumzia mradi wa ngapa ulipofikia hadi sasa.
Kwa mujibu wa waziri Mbarawa, amesema serikali imetoa shilingi bilioni mbili nukta sita kwa ajili ya kusambaza miundombinu ya maji katika manispaa ya lindi.

No comments:
Post a Comment