Msemaji wa Klabu ya Yanga, Dismas Ten ametoa wito kwa mashabiki na wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa katika mchezo wa marudiano dhidi ya Gor Mahia ya nchini Kenya.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Ten amesema kuwa Mchezo utakapigwa siku ya Jumapili katika Dimba la Uwanja wa Taifa ambapo utaanza majira ya saa moja usiku.
Katika muendelezo wa Michuano hiyo ya Shirikisho barani Afrika mpaka sasa Yanga haijafanikiwa kupata ushindi hata mmoja katika Kundi D lenye timu za USMA Alger ya Algeria, Gor Mahia ya Kenya, Rayon Sports ya Rwanda.
Mchezo uliopita julai 18 nchini Kenya mwaka huu, Yanga haikuweza kufurukuta dhidi ya Gor mahia ambapo ilikubali kichapo cha mabao 4-0
Rekodi hiyo mbaya kwa Yanga imewafanya klabu hiyo ibiruze mkia katika kundi lao kwa alama 1, wakati vinara wa Kundi hilo wakiwa Gor Mahia wenye alama 5, wakifatiwa na Rayon Sports ya Rwanda alama 5, huku nafasi ya tatu ni USMA Alger akiwa na alama 4.
"Kikosi kimekita kambi yake Mkoni Morogoro na leo walikuwa mazoezini katika uwanja polisi katika mandalizi ya mechi hiyo, Wachezaji wameaahidi kushinda kuondoka na alama nyumbani 3 ili kufika pazuri zaidi "amesema Ten
No comments:
Post a Comment