KIUNGO mshambuliaji chipukizi wa Simba, Rashid Juma, amesema kuwa upana wa kikosi chao unawapa nafasi kubwa ya kutwaa Kombe la Kagame.
Simba imemaliza Kundi C la michuano hiyo ikiwa kinara na pointi zake saba sawa na Singida United.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Juma alisema kikosi chao kina wachezaji wengi wazuri, hivyo ni kazi kwa kocha kupanga kikosi ambacho kitaanza ila ana imani kila mchezaji yupo vizuri ndani ya timu.
“Timu ya Simba kwa sasa siyo ya kuibeza kwa kuwa imekamilika na kila idara kuna wachezaji wazuri ambao wamesajiliwa, kupata nafasi ya kucheza ni chaguo la mwalimu mwenyewe mimi sina mashaka na suala la namba kwa kuwa kazi yangu ni kucheza na nikipata nafasi ni lazima nifanye maajabu.
“Mashindano ya Kagame itakuwa ni nafasi nyingine kuweza kuonyesha uwezo hasa kwa kuwa kitu kikubwa ambacho tunategemea ni kuibuka na ubingwa wa michuano hii, naamini hili linawezekana kwa kuwa tuna malengo na nia yetu ni thabiti kabisa,” alisema Juma.

No comments:
Post a Comment