Mashabiki wa timu ya taifa ya Colombia wameungana katika kuipokea timu yao katika viwanja vya mji mkuu Bogota ilipowasili kutoka nchini Urusi licha ya taarifa ya vitisho kwa wachezaji wake kusambaa.
Timu ya Colombia iliwasili nchini kwao usiku wa kuamkia leo, baada ya kuondolewa na Uingereza kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la Dunia na kukuta maelfu ya mashabiki waliojitokeza kuilaki timu yao.
Tukio hilo limeelezea namna ambavyo mashabiki hao walivyoamua kuungana na kusahau kuhusu hasira walizokuwa nazo baada ya wachezaji wao wawili Mateus Uribe na Carlos Bacca kukosa mikwaju ya Penalti iliyopelekea timu yao kuondolewa .
Baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Uingereza, zilianza kusambaa jumbe mbalimbali katika mitandao ya kijamii zilizolenga kuwatishia maisha wachezaji hao wawili na wengine wakiwataka wachezaji hao wasithubutu kurejea nchini kwao watauwawa.
Nahodha Radamel Falcao akiongea na mashabiki hao kwa niaba ya wachezaji wenzake alisema ''Mwamuzi alituangusha sana kwenye mchezo ule ambao ulikuwa 50-50, mara nyingi alionesha kuipendelea zaidi Uingereza . Hali hiyo ilituvunja moyo sana sisi, hakufanya usawa kwa timu zote kiukweli''.
Uingereza itacheza mchezo wake wa robo fainali hapo kesho dhidi ya Sweden ambayo iliiondoa Uswisi katika hatua ya 16 bora kwa ushindi wa 1-0.
No comments:
Post a Comment