Klabu ya soka ya Singida United imechukua nafasi ambayo awali ilikuwa ya Yanga kwenye michuano ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, baada ya Wanajangwani hao kujitoa na CECAFA kuamua kuipa nafasi timu hiyo kutoka mkoani Singida.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga, klabu hiyo imeupokea mwaliko wa Shirikisho la soka kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na leo inaingia kambini kuanza maandalizi ya michuano hiyo inayoanza Juni 29.
Singida United itaungana na timu zingine za Kundi C ambazo ni Simba SC, APR ya Rwanda na Dakadaha ya Somalia. Kundi A linabaki na timu za Azam FC ya Dar es Salaam, ambao ndiyo mabingwa watetezi, Vipers ya Uganda, JKU ya Zanzibar na Kator FC ya Sudan Kusini.
Kundi B litakuwa na timu za Rayon Sport ya Rwamda, Gor Mahia ya Kenya, Lydia Ludic ya Burundi na Ports ya Djibouti. Mechi za ufunguzi zitachezwa Ijumaa ya Juni 29, kati ya JKU na Vipers Saa 8:00 mchana, Azam FC na Kator Saa 10:00 jioni na Singida United dhidi ya APR Saa 1:00 usiku Uwanja wa Azam Complex.
Mechi zingine zitapigwa Jumamosi ya Julai 30, ambapo jumla ya mechi mbili zitapigwa kati ya Ports dhidi ya Lydia Saa 8:00 mchana na Simba dhidi ya Dakadaha Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa.

No comments:
Post a Comment