Wednesday, April 4, 2018

TUZO YA MCHEZAJI BORA WA ELP NI YA KELVIN DE BRUYNE AU MOHAMED SALAH

VITA  kubwa  kwenye Ligi Kuu ya England sasa imehamia kwenye tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi hiyo am­bapo wanaume wawili wana­pambana vikali.

Vita hiyo ipo kati ya kiungo wa Man­chester City, Kevin De Bruyne, na mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah na mashabiki wa soka wamekuwa waki­gawanyika kwa kiasi kikubwa kutambua nani anaweza kutwaa tuzo hiyo.

Tayari De Bruyne, ameshaonyesha hofu yake juu ya mshambuliaji huyo wa Liverpool anayeon­goza kwa kupachika mabao kwa sasa kwenye Ligi Kuu ya England.

Mbelgiji huyo ameshasema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuwa Salah atachukua tuzo hiyo kutokana na kasi yake tan­gu alipotua Liverpool mwanzoni mwa msimu huu.

Salah ni kinara kwa kupachi­ka mabao kwenye ligi hiyo ak­iwa amefunga mabao 29 huku akionekana kutawala pia kwenye ligi zote kubwa barani Ulaya kuto­kana na mabao mengi aliyofunga.

De Bruyne ambaye amekuwa nguzo sahihi kwenye kikosi cha City msimu huu ambacho kinajiandaa kutwaa ubingwa wa ligi

hiyo ameshasema kuwa itakuwa vigumu sana kwake kumzuia Salah lakini kwa kuwa ni tuzo kila kitu kinawezekana.

Tuzo ambazo zina­wania na mastaa hao ni mbili, moja ya mchezaji bora wa mwaka wa Ligi Kuu England na ny­ingine ni mchezaji bora wa mwaka wa waandishi wa habari za soka.

Vita hii imekuja wakati ambapo mastaa hao wawili watakutana kwenye mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Dimba la Anfield.

Liverpool leo watakuwa wenyeji wa Man City kwenye mchezo huo ambao unaonekana utakuwa mgu­mu sana kwa timu zote mbili.

“Ndiyo kama mimi ndiye nita­pata tuzo ya Mchezaji Bora wa England litakuwa jambo zuri sana, lakini nafikiri kwanza kwa ajili ya timu.

“Kwa njia moja nafikiri kuwa nastahili kwa kuwa nimekuwa kwenye kiwan­go kilekile kwa muda mrefu.

“Nina furaha sana mwenyewe na nime­kuwa navutika sana kwa jinsi ambavyo nime­kuwa nikicheza msimu huu.

“ Nafikiri hakuna mch­ezo ambao kiwango changu kilikuwa chini, lakini ni vye­ma nikawa na hofu na mpinzani wangu kwa kuwa ame­kuwa bora kwa muda mrefu na amekuwa mfungaji mzuri, hali­takuwa jambo rahisi kuitwaa.

“Salah amekuwa kwenye kiwan­go cha juu sana kwa kipindi cha hivi karibuni na amecheza vizuri kwenye michezo aliyocheza.

“Kitakwimu ni ngumu kunil­inganisha naye, lakini kwa kuwa ni tuzo basi ngoja tuone mwisho utakuwaje,”alisema kiungo huyo wa City.

De Bruyne ndiye kinara wa pasi kwenye Ligi Kuu ya England na Ulaya kwa ujumla akiwa amefani­kiwa kutoa pasi 15 zilizozaa mabao ambazo ni nyingi kuliko mchezaji mwingine yoyote msimu huu.

Salah yeye anakwenda kwenye tuzo hiyo akiwa na rekodi nzuri ya kupachika mabao akiwa ndiye ki­nara kwa sasa Ulaya nzima baada ya kufunga mabao 29 akifuatiwa na Lionel Messi mwenye mabao 26.

City wanakwenda kwenye Dimba la Anfield, wakitambua kuwa Liver­pool ndiyo imekuwa kizuizi chao msimu huu kwani ndiyo timu pe­kee ambayo imefanikiwa kuwafun­ga kwenye Ligi Kuu England hadi sasa wakiwa wamepoteza mchezo mmoja tu.

Mbali na kuwafunga Liverpool, wamekuwa kwenye kasi nzuri sana msimu huu wakiwa wanaamini kuwa wanaweza kumaliza kwenye nafasi ya pili mbele ya Manches­ter United ambao nao wamekuwa wakiwania nafasi hiyo.

 Baada ya City kumaliza mchezo huu wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaibuka na ushindi kwenye mch­ezo ujao wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Manchester United ili wat­wae ubingwa wa Ligi Kuu England na kwenda kwenye mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiwa hawana mawazo sana.

No comments:

Post a Comment