1. Pombe na kahawa.
Pombe na kahawa au vinywaji vingine vyenye caffeine vinaweza kuleta matatizo kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na kwa mtu asikuwa navyo anaweza kupata, hivyo ni vyema kuepuka au kutuma kwa kiasi kidogo vinywaji hivi. Kimsingi vinywaji hivi huongeza aside tumboni na hivyo vinaweza kusabbisha vidonda au kusidisha maumivu kwa anayeumwa.
2. Ulaji wa chumvi.
Utafiti uliowahi kufanywa nchini marekani umeonesha kuwepo kwa uhusiano kati ya ulaji chumvi na vidonda vya tumbo. Mgonjwa wa vidonda vya tumbo anashauriwa kuepuka kula wa vyakula vyenye chumvi nyingi, hususani vyakula vya kusindika ambavyo huweka chumvi nyingi ili visiharibike haraka. Pia jiupeshe na kuongeza chumvi mbichi kwenye chakula ambacho unakula.
3. Vyakula vyenye viuongo vingi.
Endapo kama una vidonda vya tumbo epuka kula vyakula ambavyo vina wingi wa viungo mbalimbali, mfano wa viungo hivyo ni kama vile pilipili, kwani inasadikia ya kwamba ulaji wa pilipili kali, huongeza kasi ya maumivu ya vidoda vya tumbo.
No comments:
Post a Comment