Tuesday, September 5, 2017

TUNDU LISSU AIKANA HABARI YA KUALIKWA KWENYE MKUTANO WA WANASHERIA BINGWA DUNIANI

Rais wa  (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameikana taarifa inayosambaa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kuwa amealikwa kwenye Mkutano wa Mawakili Bingwa wa sheria nchini Marekani na kusema yeye mpaka sasa hajapata mwaliko huo.

Tundu Lissu alisema hayo  jana baada ya kutoka mahakamani katika kesi yake ya uchochezi ambapo alisema kuwa hata yeye anaona taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii na kusema hajapata huo mwaliko na kudai anasubiri.

"Mimi mwenyewe nimesikia nimealikwa sehemu fulani wakili pekee barani Afrika bado nausubiri huo mualiko sijauona bado ila nimeusikia mtandaoni, sijui watu ambao huwa wanasambaza uongo kama huu inawasaidia nini, mimi naona inanipandisha 'chat' nisizo stahili mimi nataka nipande 'chat' nazostahili " alisema Tundu Lissu

Katika taarifa hiyo ambayo imesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii  ilikuwa inasema kuwa Mwanasheria huyo wa CHADEMA ni wakili pekeee kutoka barani Afrika ambaye atahudhuria Mkutano wa Mawakili Bingwa wa Sheria nchini Marekani utakaofanyika katika Jiji la Washington DC siku ya Ijumaa ya tarehe 15/09/2017

No comments:

Post a Comment