Tuesday, September 5, 2017

TFF YAITUNUKU AZAM FC

Klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, imeishukuru Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kusema wanaishukuru kwa kuweza kuwapa haki zao ambayo waliyokuwa wanayostahili kwa kipindi kirefu.

Hayo yameelezwa na taarifa iliyotolewa na uongozi wa timu hiyo kupitia ukurasa wao maalum wa facebook baada ya TFF kufanya mabadiliko ya ratiba mpya ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kuweza kuonyesha mechi zote za timu ya Azam FC ambazo atakuwa nyumbani dhidi ya Simba na Yanga zitafanyikia kwa mara ya kwanza ndani ya uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi Jijini Dar es Salaam.

"Tunaishukuru TFF kwa kutupa haki yetu hii muhimu tuliyokuwa tukistahili muda mrefu", ilisema taarifa hiyo.

Katika hatua nyingine, Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema maamuzi hayo yamefikiwa ili kuipa Azam FC haki yake katika kuutumia uwanja huo ambao unachukua idadi ya mashabiki 7,000 waliokaa kwenye siti.

"Kitakachofanyika ni kuuza tiketi zitakazotosha kwa idadi ya siti na hazitauzwa zaidi ya idadi halisi ya siti zilizopo uwanjani, hivyo wale watakaokosa watatakiwa kutosogea uwanjani kwa kuwa ulinzi utakuwa mkubwa", alisema Alfred

Kwa upande mwingine, timu ya Azam FC inatarajiwa kushuka dimbani siku ya Jumamosi Septemba 9 mwaka huu kuminyana na Simba SC katika uwanja wake wa nyumbani Chamazi
.

No comments:

Post a Comment