Monday, September 11, 2017

NANDY AFUNGUKA BIFU LAKE NA RUBY

 Nandy.

MSANII wa Bongo, Faustina Charles ‘Nandy’ amesema kuwa, japo watu wengi wamekuwa wakijadili kuhusu ukaribu wake na msanii wa zamani zao la Jumba la Kuibua Vipaji (THT), Ruby kwa madai kuwa kwa sasa hawapikiki chungu kimoja kutokana na ushindani uliopo baina yao, ishu hiyo si kweli kwani hana bifu na mwanadada huyo.
Ruby.

Nandy  anawashangaa wanavyosema hapatani na Ruby kwa madai kuwa anachukiwa kwa sababu amemfunika mwenzake kimuziki.

“Ukiniuliza mimi na Ruby nani anaimba vizuri, nitakujibu wote, yeye ana muziki wake nami nina wangu, sina ugomvi wala mazoea naye ila tukukutana tunasalimiana tu kama washikaji,” alisema.

No comments:

Post a Comment