AZAM WATALIPIZA KISASI KWA KAGERA
Katika kugombea nafasi hiyo, Kagera waliwanyong’onyesha Azam baada ya kuwachapa 1-0 katika Uwanja wao wa Chamazi, kisha wakachukua nafasi ya tatu na kuwaacha Azam wakiwa kichwa chini.
Kagera wanarudi tena Chamazi huku wakiwa na kumbukumbu ya kutoka na pointi tatu uwanjani hapo, lakini kikosi chao kikiwa na majeruhi watatu George Kavila, Jafari Kibaya na Mohammed Fakhi, huku Azam wakiwa wanataka kufuta uteja wao na kulipiza kisasi.
Azam imebadilika msimu huu, imekuwa timu yenye vijana wengi ambao wana uchu kama ilivyo kwa Kagera Sugar.
Kombinesheni ya wachezaji wa Kagera inaonekana kuungana zaidi baada ya kuwa na kocha bora wa msimu uliopita, hata Azam Kocha Aristica Cioaba, naye amejaribu kutengeneza vijana wake kwa ajili ya kufuta makosa ya msimu uliopita.
Tutarajie kuona mechi ya kukamiana katika uwanja wa Chamazi, hii sio mechi ya kuibeza hata kidogo, kwa sababu vikosi vyote vina nyota ambao walifanya makubwa kwenye vikosi vyao msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment