Friday, September 15, 2017

KOREA KASKAZINI LAFANYA JARIBIO,LAPITIA JAPAN

Korea Kaskazini imefanya jaribio jingine la kombora lililopita kwenye anga ya Japan Alhamisi Septemba 14 saa nne usiku saa za kimataifa (sawa na Ijumaa asubuhi Septemba 15 saa za Tokyo). Kombora hilo lilirushwa kupitia kisiwa cha Japan cha Hokkaido, kwa mara ya pili katika muda wa wiki tatu.


Kombora hilo lilianguka katika bahari ya Kaskazini mwa Pasifiki. Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe alizungumzia kuwa kitendo cha Korea Kaskazini ni "tishio kubwa na la kipekee". Wakati huo huo, Korea Kusini pia imehukumu kitendo hicho, na imejibu mapema asubuhi hii kwa zoezi la kurusha kombora baharini. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana haraka Ijumaa saa 7 jioni saa za kimataifa kuzungumzia hali hiyo.

Kombora la Korea Kaskazini lilirushwa karibu na uwanja wa ndege wa Pyongyang, mji mkuu wa Korea KAskazini, amearifu mwandishi wa RFI katika mji wa Seoul, Frédéric Ojardias. Kombora hilo lilirushwa kupitia anga ya kisiwa cha Hokkaido, nchini Japan, kabla ya kuanguka kaatika bahari ya Kaskazini mwa Pasifiki. Kwa mujibu wa Korea Kusini, kombora hilo liliruka kwenye urefu wa kilomita 770 na kusafiri kilomita 3,700. Jaribio hilo ni mafaanikio makubwa kwa Korea Kaskazini. Ni kombora kubwa zaidi liliyopata mafanikio makubwa Korea Kaskazini. Makombora mawili yanayokwenda hadi bara jingine yaliyofyatuliwa mwezi Julai yalikwenda juu lakini si mbali sana.

Kuimarisha shinikizo kwa Korea Kaskazini

Jaribio hili jipya linakuja wakati ambapo Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe anazuru India, ambapo Alhamisi aliomba tena kuongeza shinikizo kwa Korea Kaskazini. Waziri wa Ulinzi wa Japan, Itsunori Onodera, na Katibu Mkuu wa Serikali, wamekua wakijianda kufungua kikao cha Baraza la Usalama la Taifa kujadili kitendo cha Korea Kaskazini.

Hii ni mara ya pili ndani ya mwezi mmoja Korea Kaskazini inarusha kombora kupitia rasi ya Japaninavuka juu ya visiwa. Kombora la hivi karibuni lililopita kaskazini mwa Japan lilirusha tarehe 29 Agosti. Wakati huo huo, Korea Kaskazini pia ilifanya jaribio la nyuklia la sita tarehe 3 Septemba.

Jaribio hili ni jibu la Korea Kaskazini kwa mzunguko wa nane wa vikwazo vilivyopigiwa kura kwa kauli moja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu mjini New York baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine jipya la nyuklia.

EU yapitisha vikwazo vya Umoja wa Mataifa

Umoja wa Ulaya pia uliimarisha siku ya Alhamisi vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini, kwa kupitisha hatua zilizotangazwa mwezi Agosti 2017 na Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na jaribio la kombora la masafa marefu linalokwenda hadi bara jingine (ICBM) lenye uwezo wa kwendahadi kaskazini mwa Marekani.

No comments:

Post a Comment