Jiji la Dar es Salaa, limedaiwa linaongoza kwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya milioni sita, ukilinganisha na majiji mengine.
Hata hivyo, makadirio ya idadi ya watu katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa mwaka 2016 yalikuwa ni watu 5,465,420; wanaume 2,661,979 na wanawake 2,803,442.
Makadirio haya yametokana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 kwa kutumia mbinu za kidemografia zinazohusisha mabadiliko katika viwango vya uzazi, vifo, uhamaji na uhamiaji katika ngazi ya taifa, mkoa na wilaya/halmashauri husika.
Mradi huo ulielezwa utazisaidia halmashauri tano za Ilala, Temeke, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni ambazo zinaongezeko la watu na kukua kwa kasi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Grace Maghembe alisema Tanzania imejizatiti kufikia asilimia 40 katika uzazi wa mpango ifikapo mwaka 2020, hivyo uwapo wa mradi huo utasaidia kuongeza nguvu ya hatua iliyofikiwa sasa ya asilimia 32.
“Hatukatazi watu kuzaa, hapana. Uzazi wa mpango unamaanisha tuzae watoto tunaoweza kuwahudumia na mama apate muda wa kulea mtoto mmoja baada ya mwingine,” alisema.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita alisema ni vizuri kila mtu kuwa na watoto wachache ili aweze kuwahudumia
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Janeth Mgamba alisema mradi huo unalenga maeneo ya miji.
No comments:
Post a Comment