Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk. Joel Bendera ameyasema hayo wakati akizungumza na katika mkutano mkuu na wanachama wa Chemba ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Mkoa wa Manyara.
Amesema amepokea maagizo kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Biashara kuwataka wafanyabiashara kuandika barua ya kuomba vibali vya kuuza tena shehena zao za viroba walivyokuwa wamenunua kabla serikali haijapiga marufuku uingizaji na uuzaji.
“Nimepata maagizo kuwa wafanyabiashara wote wenye shehena za viroba muandike barua ya kuelezea idadi kamili ya viroba ulivyonavyo na andika barua eleza una kiasi gani kama una bohari zima, eleza kiasi ulichokuwa nacho halafu omba utaratibu wa kupakia upya ili ushughulikiwe, wizara inatoa vibali na wanakuruhusu na ikiwezekana hizo barua zipitie TCCIA na nakala kwa Mkuu wa mkoa,” amesema Dk. Bendera.
Pamoja na mambo mengine, amewaomba viongozi wa TCCIA kwa kushirikiana na Serikali kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu ulipaji wa kodi na tozo zingine kwani kwa kufanya hivyo kutaharakisha maendeleo kwa wanachi.
Naye Makamu wa Rais wa TCCIA Taifa, Octavian Mshiu ameiomba Serikali ya Mkoa kutenga eneo la viwanda litakalouzwa kwa bei nafuu kwa wafanyabiashara ili waweze kujenga viwanda vitakavyoongeza ajira na kutii agizo la rais la uanzishwaji wa viwanda nchini.
No comments:
Post a Comment