Wednesday, August 9, 2017

NUH MZIWANDA :SITAKI TENA WANAWAKE


Msanii wa bongo fleva, Nuh Mziwanda amefunguka na kudai hataki kusikia tena habari za wanawake kwa sasa kwa kuwa yeye ni 'single boy'.

Mziwanda ameeleza hayo kupitia kipindi cha 5seleKt kutoka EATV baada ya kupita siku chache tokea aachane na mke wake waliofunga ndoa anayefahamika kwa jina la Nawal.

"Sasa hivi nipo 'single boy' sitaki mambo ya wanawake yaani staki hata kusikia",amesema Mziwanda.

Hata hivyo, Nuh amesema japokuwa wameachana na mke wake lakini bado anaendelea kumtunza mtoto wake kwa kila hali.

"Nilitamani sana mtoto wangu ning'ekaa naye mimi 'since' yupo mdogo lakini nashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya umri wake haujifikia kukaa na baba kwa hiyo nimemuachia mama yake kwa sasa lakini kama nikiona mwanangu wanamfanyia vitu ambavyo si sawa kwangu nitaenda kumchukua nikae naye mimi mwenyewe", amesisitiza Mziwanda.

Kwa upande mwingine, Nuh amedai amempa muda wa kumchunguza mzazi mwenzake kama ataweza kuishi na mtoto wao vizuri na endapo atabaini kasoro zozote basi atamchukua na kukaa naye mwenyewe.


No comments:

Post a Comment