Wednesday, August 23, 2017

IGP SIRRO:POLISI HAITUMIKII SIASA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Siro, amejibu tuhuma zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa jeshi la polisi linatumika kisiasa na kuwaonea viongozi wa vyama vya upinzani, na kusema kuwa hakuna ukweli wowote juu juu ya hilo.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, IGP Sirro amesema jeshi la polisi halimkamati mtu kwa sababu ni kiongozi wa chama cha siasa au ni kiongozi wa dini, bali humkamata mtu iwapo kuna taarifa za uhalifu zilizowafikia kwani halifuati siasa., hivyo jukumu lao ni kuhakikisha usalama wa nchi.

“Polisi hakamati viongozi wa siasa, polisi hakamati viongozi wa dini, polisi anakamata mhalifu, na mhalifu anapomkamata anamhoji kama kuna ushahidi anampeleka mahakamani, kama hakuna ushahidi anamuachia”, alisema IGP Sirro.

IGP Sirro aliendelea kwa kuwataka wananchi wamuache afanye kazi yake kwani yeye ndiye anayewajibika na kusimamia amani, na kusema endapo utakamatwa na kukutwa hauna hatia, hawatasita kukuchia huru.

No comments:

Post a Comment