Kocha wa Gor Mahia FC, Dylan Kerr, ameelezea masikitiko yake namna alivyofukuzwa kazi na Uongozi wa Simba, baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, wakati akiifundisha timu hiyo, miezi 16 iliyopita, huko Zanzibar.
Kerr amesema mipango yake ilikuwa ni kuhakikisha Simba inatwaa ubingwa Ligi Kuu Bara na kama ikishindikana basi amalize akiwa nafasi ya pili.
Kocha huyo amesema kamwe hatawasahau mashabiki na wachezaji wake kwa ukarimu waliomuoneshea wakati akiinoa klabu hiyo, pamoja na kuiamini kazi yake huku akisema atazidi kuwakumbuka.
Kerr amewataja wachezaji baadhi kama Jonas Mkude, Vincent Angban, Peter Manyika, Justice Majabvi, Mohammed Zimbwe au Tshabalala, Mwinyi Kazimoto, kuwa ni mara nyingi amekuwa akiwasiliana nao toka aondoke Simba.
Mwisho kabisa Kerr amewataka wanasimba wote kuendelea kuonyesha umoja ndani ya timu yao, kama kauli mbiu ya Nguvu Moja, namna inavyosema.
Kocha huyo alionekana kuwa kipenzi cha wachezaji wakati akiinoa Simba lakini viongozi hawakufurahishwa naye na walisema hakukuwa na nidhamu ndani ya kikosi chake.
No comments:
Post a Comment