Tuesday, July 11, 2017

DONALD NGOMA AENDA KUTIBIWA SAUZ

Mshambuliaji wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma.

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mzimbabwe, Donald Ngoma, atachelewa kujiunga na timu hiyo baada ya madaktari kumhitaji kwa ajili ya kumfanyia vipimo vya mwisho kwenye goti lake. Mzimbabwe huyo, hivi karibuni aliongeza mkataba wa miaka miwili Yanga.

Ngoma alipata majeraha hayo msimu uliopita wa ligi kuu na kusababisha ashindwe kuitumikia timu yake kwa asilimia kubwa.

Akizungumza na Championi Jumatatu, bosi mkubwa wa timu hiyo, alisema mshambuliaji huyo ameutaarifu uongozi kuwa atachelewa kutokana na kupitia Afrika Kusini ‘Sauz’ alipokwenda kufanyiwa vipimo hivyo. Bosi huyo alisema, mshambuliaji huyo kikubwa anataka aanze ligi kuu akiwa fiti kwa kuhofia kujitonyesha.

“Ngoma atachelewa kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake kutokana na kwenda Sauz katika vipimo vya mwisho vya goti lililokuwa likimsumbua msimu uliopita. “Ngoma alianza matibabu hayo ya goti Sauz tangu alivyoumia kwa mara ya kwanza baada ya madaktari wa hapa nchini kushindwa kumtibu.

“Hivyo madaktari hao wamemhitaji tena kwa ajili ya kumfanyia vipimo vya mwisho kabla ya kumruhusu kuanza kucheza soka,” alisema bosi huyo. Ngoma alikosa sehemu kubwa ya msimu uliopita kutokana na tatizo hilo la goti.

No comments:

Post a Comment