Na. Ahmad Mmow, Kilwa.
MKUU wa wilaya ya Kilwa,mkoa wa Lindi, Christopher Ngubiagai amewataka watendaji na watumishi wa umma wilayani humu kuzingatia misingi ya utawala bora katika kuwahudumia wananchi.
Ngubiagai alitoa agizo hilo katika kitongoji cha Miembe Miwili katika mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko, alipozungumza na wananchi wa kitongoji hicho jana.
Mkuu huyo wa wilaya ambae alikuwa anahitimisha ziara zake za mwezi Julai mwaka huu, alisema katika ziara hizo amebaini kwamba wananchi wamekuwa na malalamiko ya msingi ambayo kwakiasi kikubwa yanachangiwa na baadhi ya watendaji kutozungatia utawala bora. Ikiwamo kutowashirikisha wananchi katika kufanya maamuzi ya mambo yanayowahusu.
Ngubiagai alibainisha kwamba miongoni mwa misingi mikuu ya serikali za mitaa (SMS) niushirikishaji wa wananchi katika mambo yanayo wahusu. Hatahivyo baadhi ya watendaji wamekuwa wakienda na kutenda kinyume. Hasa katika vijiji, na kusababisha migogoro isio nasababu za msingi. shirikishi .
"Kwakweli wananchi wangekuwa wanashirikishwa kusingekuwa kuwa na malalamiko mengi kiasi cha mimi kufikishiwa kwenye ziara zangu na ofisini. Niwe mkweli kwamba watendaji na watumishi wa aina hiyo hawana nafasi katika serikali hii ya awamu ya tano ambayo imelenga kuwahudumia wananchi wake bila ubaguzi, "alionya Ngubiagai. Huku akibainisha kwamba hakuna sababu za msingi kwa watendaji kutowashirikisha wananchi wakati wanajua mamlaka iliyopo ni wananchi wenyewe.
Akionesha dhahiri kukerwa na tabia hiyo, alisema kutowashirikisha wananchi ni miongoni mwa sababu zinazosababisha kutokufikiwa malengo ya mipango ya maendeleo . Hivyo mtendaji asiefanikisha kufikiwa malengo anadhihirisha kuwa hatoshi kwa nafasi hiyo.
"Sasa kama hutoshi husitahili kubaki katika utumishi wa umma. Ukitimuliwa usimlaumu mtu, kwanini ushindwe kuitisha vikao na mikutano mikuu ili usome taarifa za mapato na matumizi ili wananchi wenyewe waibue miradi ya maendeleo, "alihoji.
Katika kuhakikisha agizo lake linazingatiwa na kufanyiwa kazi, amewataka watendaji kuweka taarifa za mapato na matumizi ya vijiji, kata na hata halmashauri ya wilaya kwenye mbao za matangazo zitakazo onesha thamani na aina ya miradi inayotekelezwa katika maeneo yao, kuitisha mikutano mikuu na vikao vilivyoainisha kwa mujibu wa sheria.,
"Kwenye ziara hizi nimebaini mambo mengi sana. Hamshirikishwi katika kujua vyanzo vyenu vya mapato, tozo mbalimbali na usafirishaji wa mazao ya uvuvi, kilimo na uvuvi. Wanafanya kama miradi yao, hatuwezi kuwavumilia, wenye tabia hiyo wajisndae kuondoka na tukigundua ufisadi tunawakifisha kwenye mikono ya sheria, "alionya.
Wilaya ya Kilwa ni miongoni mwa wilaya za mkoa huu ambazo baadhi ya vijiji vyake vimekuwa na migogoro ya mara kwa mara inayotokana na baadhi ya watendaji na viongozi kushindwa kuwashirikisha wananchi katika mambo yanayowahusu Ikiwamo taarifa za miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.

No comments:
Post a Comment