Watu waliofariki dunia, waliohama na wasiofahamika wilayani Rorya mkoani
Mara, wamemchanganya mkuu wa wilaya hiyo Simon Chacha kuendelea
kunufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini.
Mpango huo ambao unaendeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf),
umebaini wati 112 wasiotakiwa kunufaika nao, lakini walikuwa wakivuna
fedha za ruzuku kila zitolewapo.
Chacha amesema kuanzia sasa hataki kusikia kwamba kuna watu wa aina hiyo
ambao wanatumia jasho lisilowahusu kunufaika nalo na kwamba, hatua kali
zitachukuliwa kwa watakaobainika.
Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo wakati wa ziara ya kutembelea kaya
maskini katika Kijiji cha Nyabikondo kilichopo Kata ya Kinyeche na
Kijiji cha Ryaghati katika Kata ya Nyahongo wakati wa utoaji na upokeaji
fedha kwa kipindi cha Machi na April 2017, mwaka huu.
Akiwa Kijiji cha Nyabikondo, Chacha alihoji baadhi ya wananchi
wanaonufaika na fedha ambapo alibaini baadhi ya majina ya walengwa
waliofariki akiwamo Victoria Obimbo ambaye alikuwa akipokea ruzuku ya
Sh20,000 na alifariki mwezi Januari, 2017 lakini fedha zake zinaendelea
kuchukuliwa na ndugu yake.
“Naombeni kama mnajua kuna watu walifariki na majina yao yanaendelea
kupokewa fedha semeni, haiwezekani pesa ilikuwa inatolewa kwa mlengwa
husika halafu akafariki, lakini wanamchukulia pesa mtu akishafariki na
mgao wake unakuwa umekoma,” amesema Chacha
Baadhi ya wanufaika akiwamo Sophia Ochora wamelalamika kuku kufa kwa
ugonjwa na mwingine Julia Majengo amedai kondoo wake wawili waliliwa na
hivyo ndoto zake kutotimia.
Mratibu wa Tasaf wilayani Rorya, Ayoub Mrimi amesema kuwa wamepokea
fedha za kaya maskini Sh254 milioni zitakazonufaisha vijiji 52 kati ya
vijiji 87 vyenye kaya 7,241 zilizothibitshwa kuingizwa kwenye mpango
huo.
No comments:
Post a Comment