Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo amefika mbele ya kamati
ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kufuatia wito wa Kamati hiyo kumtaka
afike mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki,
Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi aliyoyatoa mapema mwezi
februari 2017 jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na madai ya kudharau
Bunge.
Wito
wa kufika mbele ya Kamati hiyo unafuatia Azimio la Bunge lilitolewa
tarehe 8 Februari 2017 ambapo Bunge liliazimia Mhe. Spika aweze kukubali
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Alexandra Mnyeti na Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam Mhe. Mhe Paul Makonda wahojiwe kutokana na Matamshi yao ya
Kudharau Bunge.
No comments:
Post a Comment