Aliyekuwa Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassani Dalali ‘Trump’, ametamka kuwa kama uongozi wa timu hiyo ukifanikiwa kumsainisha mkataba kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima basi wamekwisha.
Kauli hiyo, ameitoa ikiwa ni siku chache baada ya taarifa kuenea kuwa kiungo huyo amemalizana na Simba asilimia 80 kwenye mazungumzo yao kwa ajili ya kuja kukipiga Msimbazi.
Dalali alisema Niyonzima ni kati ya viungo bora Afrika, hivyo anaamini kama akitua kuichezea Simba, basi msimu ujao wa Ligi Kuu Bara watakuwa na kikosi imara.
Dalali alisema anafurahishwa na uwezo wake mkubwa wa kuchezesha timu na kupiga pasi za mabao, hivyo ujio wake utaimarisha kikosi hicho kinachonolewa na Mcameroon, Joseph Omog.
“Ninasikia na kuona kwenye mitandao taarifa za viongozi wa Simba kuwa wapo kwenye mazungumzo ya mwisho ya kukamilisha usajili wa Niyonzima.
“Huyo ni kati ya viungo bora ninaowapenda na ninakumbuka kipindi cha uongozi wangu tulishawahi kumuhitaji kipindi hicho bado mdogo damu ikiwa bado inachemka,” alisema Dalali.

No comments:
Post a Comment