Wanafunzi wa sayansi wamehamia katika chumba maalum chenye mazingira yanayofanana na ya Mwezi ambapo watakaa kwa siku 200.
Lengo ni kuwaanda kwa safari ya kuishi kwa muda mrefu kwenye kituo cha anga za juu kwenye Mwezi, bila kupokea usaidizi wowote kutoka ardhini.
imewekeza pesa nyingi sana katika mpango wake wa anga za juu, ikilenga kushindana na Marekani an urusi.
Wanafunzi wanne wa taaluma ya anga za juu wanaosomea shahada za juu chuo kikuu cha beihang walihamia chumba hicho maalum Jumatano, ambacho kimepewa jina Yuegong-1. Maana ya jina hilo ni Kasri la Mwezi.
Watakaa katika chumba hicho maalum kwa siku 60, lakini watafuatiwa na kundi jingine la wataalamu ambao watakaa kwa siku 200 mfululizo.
Wanne hao kisha watarejea na kukaa kwa siku 105.
Shirika la habari la Xinhua linasema miongoni mwa mambo yanayofanyiwa majaribio ni uwezekano wa kuishi kwa kujitosheleza anga za juu kwa muda mrefu bila kutegemea msaada kutoka nje.
Mwaka 2016, wana anga wa China Jin Haipeng (kulia) na Chen Dong walikaa siku 30 anga za juu
Kinyesi cha binadamu kitaozeshwa kwa kutumia viumbe hai.
Mimea na mboga itakuzwa kwa kutumia taka mbalimbali za chakula na matumizi mengine.
Mpango wa kutuma watu wakakae muda mrefu kwenye Mwezi utajumuisha kutumwa kwa sehemu mbili kubwa za mtambo za kukuzia mimea, na sehemu nyingine kubwa sawa na nyumba ambao itakuwa na vyumba vinne vya kulala, sebule moja, bafu, chumba cha kubadilishia taka na chumba cha kufugia wanyama.
Ingawa mpango huo wa Kasri la Mwezi unawaandaa wana anga kukaa muda mrefu kwenye Mwezi, kwa sasa China haijapanga kutuma wana anga wengine kwenye Mwezi kabla ya miaka 10 kupita.
No comments:
Post a Comment