Thursday, May 25, 2017

MUHONGO NA UZOEFU WA KUFUKUZWA


Profesa Sospeter Muhongo 

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemuondoa Profesa Sospeter Muhongo kwenye Baraza la Mawaziri katikaakata la mchanga wa dhahabu, lakini inaonekana haikuwa kazi rahisi kwake.
Hii ni mara ya pili kwa Profesa Muhongo kuachia uwaziri huo nyeti ndani ya miaka minne, anaingia katika orodha ya mawaziri wengi wa nishati na madini waliolazimika kujiuzulu au uteuzi wao kutenguliwa.
Jana, mambo matatu yalijitokeza kwa Magufuli; alikuwa akitengua uteuzi wa waziri wa tatu tangu aunde Serikali ya Awamu ya Tano, alikuwa anamuondoa “rafiki” yake na alikuwa akimuondoa mtu ambaye hakuwahi kuona mwingine anayefaa Wizara ya Nishati na Madini zaidi yake.
Na mtiririko wa kutangaza hatua alizochukua kwa haraka baada ya kukabidhiwa ripoti ya kamati iliyochunguza sakata la kiwango cha madini kwenye makontena ulionyesha ugumu huo kwani jina la Profesa Muhongo lilikuwa la mwisho.
Rais aliunda kamati hiyo kuchunguza madini yaliyomo katika makontena 277 ya mchanga yaliyokuwa yakisafirishwa kwenda nje ya nchi kuyeyushwa kupata masalia baada ya mchakato wa kwanza wa kuondoa dhahabu mgodini.

No comments:

Post a Comment