Jana
tarehe 02, Mei 2017 tumekuwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Mh.
Humphrey Polepole ambaye amefanya ziara ya kukiimarisha chama chetu cha
mapinduzi CCM katika wilaya yetu ya Longido na kuzungumza na wanaCCM
wakiwamo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Longido, wajumbe
kamati ya siasa ya wilaya.
Mh. polepole amesema yafuatayo:
1.
Serikali imedhamiria haswaa kuimarisha sekta ya usafiri wa anga ( ATCL )
kwa kuagiza ndege zingine ili kufikia ndege saba ikiwamo ndege kubwa ya
kubeba abiria wasiopungua300, ndege tatu zenye uwezo wa kubeba abiria
102 kila moja ambazo zitasaidia kukuza sekta ya utalii nchini ili
kuliingizia taifa fedha za kigeni.
2.
Serikali italeta kwa wananchi tani 500 za chakula kwa bei nafuu ili
kuwasaidia wananchi wasio na uwezo wa kumudu bei za chakula sokoni. kwa
mujibu wa mheshimiwa Polepole Chakula hicho kitaanza kuingia juma
lijalo.
3. Tutapambana kufa na kupona ili kurejesha ccm jimbo la longido na kata zake zote zilizobebwa na wapinzani.
4.
Mradi mkubwa wa maji kusainiwa tarehe 06/05/2017 ili kuwaletea wanachi
wa longido huduma ya maji na kuwaondolea kabisa shida ya maji na tatizo
kuwa historia. Mradi huo utatoa maji kutoka West Kilimanjaro wilaya ya
Siha.
5.
Kiwanda kikubwa haswaa cha kutengeneza viatu kujengwa moshi Kilimanjaro
na kwamba wamasai sasa wajiandae kupata soko kubwa la ngozi ya ng’ombe
zitakazohitaji katika kiwanda hicho.
6.
Chama cha mapinduzi kimepanga kujenga chuo kikubwa cha uongozi kwa
ajili ya wanaccm na kwamba yeyote mwenye ndoto ya kuwa kiongozi ni
lazima apitie chuo hicho.
7.
Mheshimiwa Polepole ameguswa na Changamoto mbalimbali zinazoikabili CCM
Longido ikiwamo Kukosa Ofisi ya Chama yenye kukidhi mahitaji ya sasa na
hivyo Kuchangia Tsh. 500,000/= kwa ajili ya Shughuli za Ujenzi.
Tuungane pamoja kukijenga Chama.
8.Mheshimiwa
Polepole ametoa rai kwa Wanaccm kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa
ndani wa Chama cha mapinduzi unaendeleaje nchini kote. Ametutaka
tuchague viongozi wenye mapenzi mema na nchi yetu na Taifa kwa Ujumla,
wenye vigezo stahiki & Waadirifu. Tusiwape nafasi Watoa rushwa ambao
hutumia pesa zao kusaka uongozi. Hili halikubaliki hata kidogo.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi...Hii ndiyo ccm bwana, tukiahidi tunatekeleza. HAPA KAZI TU.
Robert PJN Kaseko
Mjumbe Baraza Kuu UVCCM (M) Arusha.
Mei 02, 2017
No comments:
Post a Comment