Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini ndiye anayejaribu kupandikiza mgogoro
ndani ya chama hicho kwa maslahi yake binafsi.
Ameyasema
hayo mapema hii leo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha 360
kinachorushwa na CloudsTv. kilichopo Jijini Dar es salaam.
Amesema
kuwa hakuna haja ya wanachama kuwa na hofu kuwa chama hicho kinaweza
kusambaratika hivyo amewataka kuimarisha mshikamano uliopo ndani ya
chama hicho.
“Nachojua
mimi hakuna mgogoro ndani ya CUF kama inavyoelezwa na baadhi ya watu,
isipokuwa Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini anajaribu kupandikiza
mgogoro huo kwa maslahi yake binafsi,”amesema Seif.
Aidha, ameongeza kuwa kuna baadhi ya watu ambao wanatumiwa kutaka kukivuruga chama hicho, hivyo amesema kamwe hawatafanikiwa.
Hata hivyo, amesema yeye kama kiongozi ataendelea kufanya shughuli zake za chama na kuwataka walio chini yake wasivunjike moyo.
No comments:
Post a Comment