Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai jana
ameonyesha aliumizwa na kitendo cha Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya CHADEMA
Mh. Halima Mdee kumwambia 'fala' bungeni na kusema hata kama mtu
humpendi lakini si vyema kumtusi matusi.
Job
Ndugai alisema hayo alipokuwa akitoa maana ya neno fala bungeni ambapo
ilibidi arejee maana hiyo kwa kusoma kupitia kamusi ya Kiswahili ambayo
ilitoa maana kuwa fala ni mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri.
"Kwa
neno ambalo alilisema Halima Mdee humu ndani, kamati imeenda kwenye
tafsiri ikachukua Kamusi kwa neno lile alilosema ambalo maana yake kwa
yule unayemwambia 'Fala' ni mtu ambaye akili zake hazifanyi kazi vizuri,
ni mtu mpumbavu, ni mtu bwege, ni mtu mjinga, ni mtu bozi, ni gulagula.
Ndiyo maana nikasema sisi Waafrika hata kama humpendi namna gani
mwenzako huwezi kumfanyia hivyo" alisisitiza Job Ndugai
No comments:
Post a Comment