Uongozi Klabu ya Azam FC, umesema kuwa
utautumia vilivyo udhamini wao kutoka Benki ya NMB kukijenga upya kikosi
chao ili siku zijazo waweze kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa.
Wikiendi iliyopita, Azam iliondolewa
rasmi kwenye kinyang’anyiro cha kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya
kimataifa baada ya kufungwa na Simba bao 1-0 kwenye mchezo wa nusu
fainali ya Kombe la FA.
Kwa muda wote ambao NMB imekuwa
ikiidhamini Azam, timu hiyo imefanikiwa kubeba Kombe la Mapinduzi pamoja
na Kagame pekee, lakini uongozi huo umesema kuwa kwenye vipengele vya
mkataba kuna sehemu wanatakiwa kukuza soka la vijana na sasa watakitumia
vyema.
Meneja wa Azam FC, Philipo Alando,
amesema hayo hivi karibuni wakati wafanyakazi wa NMB walipotembelea
makao makuu ya klabu hiyo maarufu kama Azam Complex jijini Dar na
kushuhudia maendeleo mbalimbali yanayotokana na uwekezaji huo na
kufanikiwa kucheza mechi moja ya kirafiki na kukubali kichapo cha mabao
7-2, kutoka kwa Azam U-20.
“Kiukweli mafanikio yetu yanatokana na
udhamini wetu, licha ya uchanga wetu lakini tumeweza kupambana na timu
kongwe za Simba na Yanga.
“Sasa baada ya kumudu ushindani wa ligi
ya ndani, mikakati yetu kwa sasa ni kuhakikisha tunakijenga kikosi chetu
kuwa imara zaidi ili siku zijazo tufike mbali,” alisema Alando.
No comments:
Post a Comment