Serikali yamuondoa Mkurugenzi wa UNDP nchini
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeliagiza Shirika la Umoja wa
Mataifa la Programu ya Maendeleo (United Nations Development Programs –
UNDP) kwa upande wa Tanzania kumuondoa nchini Mkurugenzi wa Shirika hilo
Bi Awa Dabo.
Serikali
ilifikia uamuzi huo kutokana na Bi Dabo kutokuwa na maelewano mazuri
na baadhi ya Watumishi wenzake na Menejimenti ya Shirika hilo, hivyo
kupelekea kuzoretesha utendaji wa shirika hilo nchini na kupunguza kasi
ya kuleta maendeleo kwa Watanzania endapo hatua za haraka
zisingechukuliwa.
Baada
ya kuthibitishiwa kuondoka nchini, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya
Nje imetoa rai kwa UNDP kuwakumbusha Watumishi wake kuwa kipaumbele chao
ni kufanya kazi na Serikali ili kufikia malengo yaliyoainishwa kwenye
Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano na
Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo yamefafanuliwa katika Agenda ya
Mwaka 2030.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasili ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 25 Aprili 2017.
No comments:
Post a Comment