Mbunge
wa Kuteuliwa, Salma Kikwete (CCM), ameeleza kushangazwa kwa kitendo cha
Serikali kukaa kimya juu ya ubadhirifu wa Sh bilioni 30 Bodi ya
Korosho.
Mke
huyo wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, alitoa kauli hiyo bungeni jana
wakati akiuliza swali la papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
“Umekuwapo
ushahidi wa kutosha kabisa kuhusiana na wizi unaofanyika kwenye
biashara ya korosho, hasa katika mikoa ya Mtwara na Lindi, ukiachilia
mbali kazi iliyofanywa na Takukuru iliyobainisha kwamba kumekuwa na
upotevu wa kiasi kikubwa cha fedha shilingi bilioni 30 kutoka Bodi ya
Korosho.
“Serikali
hatujasikia, mimi binafsi na wengine hawajasikia juu ya jambo hili. Je,
Serikali leo inatuambia nini kuhusu ubadhirifu huu uliotokea hapa
nchini kwetu, hasa wananchi wa Mtwara na Lindi kwa sababu jambo hili
linaweza kutokea sehemu yoyote nchini mwetu,” alihoji.
Akijibu
swali hilo, Majaliwa alisema mienendo ya vyama vya ushirika nchini
imeonyesha si mizuri kwa kuonyesha upotevu wa fedha na inawakatisha
tamaa wakulima.
“Mienendo
ya vyama vyetu vya ushirika nchini vimeonesha si mizuri kwa kuonesha
upotevu wa fedha na unakatisha tamaa wakulima wetu na Serikali inafanya
mapitio ya vyama vyote na tumeanza na vyama vya ushirika wa kilimo.
“Tulikuwa
na kikao Bagamoyo kwa ajili ya ubadhirifu huo wa bilioni 30 na Serikali
iliunda timu maalumu na ikagundua kuwa ni hasara ya Sh bil 6 si bilioni
30 na haikusababishwa na bodi bali vyama vikuu na vyama vya ushirika
vilivyopo kata na wilaya, vyama vya msingi na vyama vikuu na vyote
vilifanyiwa uchunguzi na hatua zimeanza kuchukuliwa,” alisema.
Pamoja
na majibu hayo ya Waziri Mkuu, Salma aliuliza swali la nyongeza akisema
haijalishi ni kiasi gani cha fedha kimechukuliwa, lakini watalipwa
lini.
“Haijalishi
ni kiasi gani cha fedha kimechukuliwa, hizi bilioni sita na hizi ni
haki za wananchi je, wananchi wanazipataje fedha hizo?” alihoji mbunge huyo.
No comments:
Post a Comment