Serengeti
Boys inajiandaa na fainali za mataifa Afrika kwa vijana zinazotarajiwa
kuanza Mei 14, mwaka huu nchini Gabon ambapo wamepangwa Kundi B sambamba
na Niger, Angola na Ethiopia.
Akizungumza
kutoka kambini nchini Morocco, Shime alisema lengo la mchezo huo ni
kuangalia mapungufu ya kikosi chake kabla ya kulekea nchini Gabon
tayari kwa mashindano hayo.
“Tunashukuru
maandalizi yapo vizuri na kila kitu kipo sawa, vijana wako na ari kubwa
kabisa na wako tayari kwa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Gabon ambao
ndiyo wenyeji wa michuano hiyo, naamini itatusaidia kujua aina ya timu
tunazoenda kucheza nazo, hivyo kwetu ni jambo zuri.
“Hii
mechi itasaidia kutambua mapungufu ya wachezaji wangu kabla ya
kurudiana nao Aprili 25 kwa sababu baada ya kucheza na Ghana nyumbani
hatukucheza mchezo wowote,” alisema Shime.
No comments:
Post a Comment