Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameagiza kuanzia sasa
miradi yote ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) itumie nguzo na
transfoma zinazotengenezwa nchini.
Alisema
hayo juzi mjini hapa wakati akizindua Bodi ya Nishati Vijijini. Alisema
ni vyema wakandarasi wa mradi huo wakafuatiliwa mahali wanaponunua
vifaa.
“Naagiza
miradi yote ya REA awamu ya tatu itumie nguzo zinazozalishwa nchini,
wakandarasi wote wanunue nguzo za Tanzania, zikiisha ndio waende nje ya
nchi,” alisema.
Alisema
tayari amepokea malalamiko kuwa nguzo zisizo na hadhi zinataka
kununuliwa na kuna nguzo nyingine hazidumu hata miaka mitatu.
“Hata
transfoma tunataka zinazotoka ndani ya nchi, kuna kampuni Wanaosambaza
chakula kibovu kushughulikiwa Muhongo azuia REA kutumia nguzo na
transfoma za nje 202750005 ya Tanalec waelekezwe wafanye uzalishaji wa
kutosha, transfoma nyingi za kutoka nje ya nchi zina matatizo,” alisema.
Pia alitaka kampuni zote za nje ambazo zitatekeleza mradi huo zifanye kazi na wakandarasi wadogo wa Tanzania.
“Lazima
wakandarasi wote wadogo wawe wa kampuni za kitanzania na kuna madai
kampuni kubwa hazilipi wakandarasi wadogo na wakandarasi wadogo hawalipi
vibarua,” alisema.
Alisema
hali hiyo imekuwa ikifanya vijana wanaofanya kazi ya kuchimba mashimo
ya kusimika nguzo katika maeneo ya vijijini kutolipwa. W
aziri
huyo aliitaka bodi hiyo kukaa na wakandarasi watakaotekeleza miradi ya
awamu ya tatu ili kujiridhisha na kila mkandarasi na kampuni yake aeleze
historia yake na hiyo kazi ataiwezaje.
Alisema
katika REA awamu ya pili wakandarasi wanane walishindwa kazi na
kuangalia kama majina yao yameingia katika miradi ya REA awamu ya tatu.
“Bodi
lazima ikae na wakandarasi watakaotekeleza miradi ya awamu ya tatu na
kila mkandarasi mjue historia yake na kama hiyo kazi ataweza. REA awamu
ya pili iliyoisha wakandarasi wanane walishindwa kazi na mpewe majina
kama wamewekwa katika awamu ya tatu,” alisema.
Waziri
Muhongo alisema lazima bodi ikae na wakandarasi hao na kuwauliza na
kuangalia uwezo wao na makampuni yao ili kujiridhisha.
“Lazima
muangalie kama ana uwezo muone, ukubwa wa bajeti, vitendea kazi
walivyonavyo na wataalam walionao ni lazima maofisa wa REA na wale wa
Shirika la Umeme (Tanesco) wawepo,” alitaka ubora wa kazi uangaliwe.
“Wabunge walipita Njombe walitutukana sana walikuta zaidi ya transfoma 20 zilikuwa zimekufa jambo kama hili halipendezi,” alisema.
Mkurugenzi
Mkuu wa Rea, Gissima Nyamo-Hanga alisema hiyo ni bodi ya nne ambapo
kila baada ya miaka mitatu bodi mpya imekuwa ikiteuliwa.
Naibu
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa James Mdoe aliwataja wajumbe wanane
wa bodi hiyo ni Mwenyekiti wake Dk Gideon Kaunda, wajumbe ni Amina
Hussein, Innocent Luoga,Michael Nyagogo, Stella Mandago, Stolastica
Jullu, Happiness Mhina na Theobard Manumbe.
No comments:
Post a Comment