Friday, March 9, 2018

UONGOZI WA KIWANDA CHA SUKARI WAFURAHIA ULINZI KUIMARISHWA ZANZIBAR

Uongozi wa kiwanda cha sukari Zanzibar kimesema kuwa kuimarishwa kwa ulinzi wa vyombo vya usalama kumesaidia kupunguza changamoto za uhujumu wa mashamba ya miwa visiwani humo hali iliyokua inasababisha kukwama kwa uzalishaji wa sukari visiwani humo.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya tenki la kuhifadhia maji kwa uongozi wa jeshi la polisi wilaya ya Kaskazini B, Unguja Meneja wa mahusiano wa kiwanda hicho Fatma Said Aliy amesema ulinzi wa vyombo vya usalama ikiwemo jeshi la polisi kumesaidia kupunguza uhalifu katika mashamba ya miwa.

Amesema kuwa awali matukio ya uchomaji moto wa mashamba ya miwa yalikua yakijitokeza mara kwa mara hali ambayo ilikua ikirejesha nyuma juhudi za uzalishaji wa sukari kiwandani hapo.

Naye Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kaskazini B Unguja Ali Ameri Haji amesema jeshi hilo litaendelea kuzidisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kutoa elimu kwa wananchi katika kuthamini uzalishaji wa miwa na kuyalinda mashamba hayo.

No comments:

Post a Comment