Kaimu Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Chunya mkoani Songwe, Benedict
Polycap amesema baadhi ya watumishi wanashindwa kufanya kazi kwa
utulivu kutokana na kipato chao kupungua baada ya kuanza kukatwa
malimbikizo ya mkopo wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.
Polycap alitoa taarifa hiyo juzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku
Galawa, kwamba hali hiyo imesbabisha baadhi ya watumishi kupokea
mishahara midogo isiyokidhi mahitaji yao hata kwa wiki mbili.
Alisema baadhi ya watumishi wanapokea mishahara kuanzia Sh100,000 hadi
Sh200,000, hivyo huamua kujiingiza kwenye shughuli nyingine kutafuta
kipato cha ziada ili kujikimu.
Katika tukio jingine, Galawa aliagiza kukamatwa mara moja kwa watumishi
wanne wanaodaiwa kugoma kuhamia Halmashauri ya Songwe na kubaki Chunya,
huku wakiendelea kupokea mishahara.
Galawa alitoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa za idara za
halmashauri hiyo. Taarifa hiyo ilibainisha kuwa watumishi wanne
hawajaripoti tangu kuanzishwa kwake Septemba 2016.
No comments:
Post a Comment