Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo imetangaza kuwa Kocha Mkuu wa kikosi
hicho, Mfaransa Thierry Froger ameachia ngazi kwa makubaliano baada ya
kuiongoza timu hiyo kwa mwezi mmoja.
TP Mazembe imeeleza kuwa sababu hasa ya kocha huyo kutema mzigo ni
kutokana na kutotimiza malengo yake ya kufika hatua ya robo fainali ya
Ligi ya Mabingwa Afrika kufuati timu hiyo kutolewa na CAPS United ya
Zimbabwe kwa faida ya bao la ugenini katika raundi ya 32.
Mabingwa mara mbili wa Ligi ya Mabingwa Afrika, JS Kabylie ya Algeria ambao waliitoa Etoile ya Congo, na kutinga hatua ya mtoano, wamepangwa kukutana na TP Mazembe.
Katika droo iliyochezeshwa Jumanne ikishirikisha washindi bora kwenye kundi la Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na timu 16 zilizopenya kutoka raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho, JS Kabylie imeangukia kwa mabingwa hao watetezi wa Kombe la Shirikisho, TP Mazembe.
Mshindi wa jumla katika mechi mbili za nyumbani na ugenini atacheza hatua ya makundi ya michuano hiyo ambayo msimu huu zitakuwapo timu 16 zitakazopangwa katika makundi manne.
Mazembe ambayo imetwaa ubingwa wa Afrika mara tano, inatumai kuteua kocha mpya kabla ya mechi hizo mbili zitakazopigwa mwezi ujao huku ikianzia nyumbani.

No comments:
Post a Comment