Chama
Cha Mapinduzi (CCM) katika kuendelea kufanya mageuzi ya uongozi, muundo
na mfumo, kimefanya uteuzi wa makatibu wa mikoa 31 wakiwamo wapya 20,
na wa wilaya 155 ambao uteuzi wao unaanza mara moja kuanzia jana.
Pia chama hicho kimekiri kufanya mabadiliko ya kikatiba yanayolenga maeneo matatu ambayo ni misingi ya uongozi, muundo na mfumo pamoja na utawala na utendaji kwa lengo la kukijenga zaidi chama hicho, na hakuna sehemu yoyote kwenye Katiba hiyo iliyobadilishwa inayohusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Akizungumza jana Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole alisema kati ya makatibu hao walioteuliwa wa mikoa 11 ni wale waliopandishwa hadhi kutokana na utendaji wao na 20 ni wapya kabisa.
Alisema katika orodha ya makatibu hao walioteuliwa, chama hicho kilizingatia sifa hizo ikiwemo maadili, weledi, jinsia na mpango wa kuachiana vijiti kwa kuzingatia rika.

- Arusha- Elias Mpanda
- Dar es Salaam- Saad Kusilawe
- Dodoma- Jamila Yusuf
- Geita- Adam Ngalawa
- Iringa- Christopher Magala
- Kagera- Rahel Degeleke
- Katavi- Kajoro Vyahoroka
- Kigoma- Naomi Kapambala
- Kilimanjaro- Jonathan Mabihya
- Lindi- Mwanamasoud Pazi
- Manyara- Paza Mwamlima
- Mara- Innocent Nanzabar
- Mbeya- Wilson Nkhambaku
- Morogoro- Kulwa Milonge
- Mtwara- Zacharia Mwansasu
- Mwanza- Raymond Mwangala
- Njombe- Hossea Mpagike
- Pwani- Anastanzia Amasi
- Rukwa- Loth Ole Nesere
- Ruvuma- Amina Imbo
- Shinyanga- Haula Kachambwa
- Simiyu- Donald Etamya
- Singida- Jimson Mhagama
- Tabora- Janeth Kayanda
- Tanga- Allan Kingazi.
“Makatibu
wengi (20) tuliowateua ni wapya, hatuwezi kufanya mageuzi ya kuwa na
CCM mpya na upya huo usionekane. Mageuzi ni fikra” amesema Polepole.
Lakini pia alisema katika orodha hiyo ya makatibu wa wilaya wa CCM 155, makatibu 76 ni wapya kutokana na vigezo vipya vilivyowekwa na chama hicho.
Aliwataja baadhi yao kuwa ni Mussa Matoroka anayekwenda Arumeru, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gaddafi’ (Longido), Joyce Mwenda (Namtumbo), Kombo Kamote (Bagamoyo), Grevas Ndaki (Momba), Othman Dunga (Hanang), Pili Augustino (Dodoma Mjini) na Martin Mwakitabu (Chamwino).
Wengine ni Aveline Ngwada (Bukombe), Nuru Ngeleja (Chato), Michael Mbaga (Iringa Mjini), Afidu Luambano (Temeke), Joyce Mkaugala (Ilala), Hanaf Msabaha (Kinondoni), Salum Kali (Ubungo), Robert Kalenge (Kigamboni), Ramadhan Dallo (Arusha) na Gulisha Mvanga (Monduli).

Kuhusu
suala la Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam, Polepole alisema, kwanza napenda
kusema kuwa uhusiano wa CCM na vyombo vya habari ni wa kihistoria’… CCM
inapenda kufuata utaratibu na ndio salama yetu kama yupo kiongozi wa
chama amefanya jambo tuna utaratibu mzuri wa kuchunguza. Lakini pili,
Mkuu wa Mkoa ni mteule wa Rais na anapomteua anamteua yeye peke yake na
halazimiki kushauriana na mtu, hivyo badala ya kukaa na kumpangia Rais
kitu cha kufanya, tumuache afanye kazi’.. “
Aidha,
Humphrey Polepole akitolea ufafanuzi madai yanayoenezwa kuwa wamefanya
mabadiliko kuwa Rais Magufuli ndiye atakayegombea 2020 bila kupingwa
amesema kuwa, mabadiliko ya katiba waliyoyafanya katika mkutano mkuu
maalum, hayakuhusu mchakato wa kumpata mgombea wa uchaguzi mwaka 2020.
Hivyo tunawaomba wanachama wetu na watanzania wapuuze habari nyingine
zinazoenezwa.
Katibu wa CCM itikadi na Uenezi Taifa
No comments:
Post a Comment