Mbunge
wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amefunguka na kusema ile hali ya polisi
kuwakamata wabunge hovyo sasa mwisho baada ya jana Ndugai kutoa uamuzi
kuwa Afisa yoyote wa Serikali ambaye atakuwa akimuhitaji mbunge ni
lazima kwanza atoe taarifa kwa spika
Hali
hii imefikia baada ya Jumatano bunge kupitisha azimio la kutaka kwanza
ruhusa ya spika wa bunge pale vyombo vya dola kama polisi wanapokuwa
wanamuhitaji mbunge yoyote kwa jambo lolote.
"Leo
(jana) Spika wa Bunge ametoa uamuzi wa Spika kwamba Afisa wa Serikali
anapomtaka mbunge kwa jambo lolote lile lazima kwanza kupata kibali
chake. Mabunge yote ya Jumuiya ya Madola hulinda kwa wivu mkubwa hadhi
yake kama mhimili. Sasa kukamata kamata wabunge hovyo mwisho. Lazima
mihimili iheshimiane. Sasa tuone kama Sirro atamfuata Mbunge wa Hai kama
alivyosema" alisema Zitto Kabwe
Mbali
na hilo Mhe. Zitto Kabwe ametoa pongezi kwa wabunge wote pamoja na
Spika wa bunge kwa kuonyesha msimamo na kupigania heshima ya bunge
"Nawapongeza
wabunge wote kwa kuonyesha msimamo katika jambo hili na ninampongeza
sana Spika Ndugai kwa kusimamia heshima ya bunge lake" Alimalizia Zitto Kabwe
No comments:
Post a Comment