Uharibifu huo wa mali ulitokea usiku wa kuamkia Jumanne ambapo watu watatu wa familia za wafugaji wakiwa na mapanga, wanadaiwa kufyeka shamba hilo lenye ukubwa wa ekari tatu.
Akisimulia tukio hilo, msimamizi wa shamba, Redio Luhanga alisema alishudia wafugaji watatu wakifyeka shamba hilo saa 12:00 asubuhi lakini alishindwa kuwadhibiti kwa kuwa walikuwa na silaha za jadi huku yeye akiwa na jembe.
Waandishi wa habari walifika kwenye shamba hilo juzi na kushudia miti ya kupandwa aina ya 'cyprus' ambayo inakadiriwa kuwa na miaka miwili ikiwa imekatwa na kuanguka Chini.
Mchele, ambaye ni mkulima na mmilki wa shamba hilo alidai chanzo cha wafugaji hao kufyeka miti yake ni uhasama uliotokana na kuwalipisha watuhumiwa fidia ya Sh. 300,000 baada ya mifugo yao kula mahindi kwenye Shamba hilo.
Mchele alisema Januari 31 msimamzi wa shamba hilo alikamata mifugo ya wafugaji hao ikila mazao katika shamba hilo, na hivyo kuita msaada wa majirani amabo waliikamata na kuchukua hatua zilizohitimishwa kwa kulipa fidia ya Sh. 300,000 Februari 6.
Lakini usiku wa kuamkia Februari 7, alisema Mchele, miti hiyo ikakatwa.
Ofisa Mistu wa kata ya Nyarugusu, Aisha Msemo alisema tukio hilo limetokea wakati serikali ikisisitiza suala la upandaji miti kwa wananchi wake ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Msemo alisema miti hiyo ingevunwa, mkulima huyo angepata Sh. milioni 150.
Jeshi la Polisi mkoani Geita limethibitishi kutokea kwa tukio hilo na kusema linawashikili watu watatu ambao ni Masanja Shigera (45), Maneno John(24) na Hamisi Daudi (18), wote wakazi wa kijiji cha Nyarugusu wilayani Geita kwa hatua za kisheria.
No comments:
Post a Comment