Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George
Simbachawene amesema kuwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanafanya kazi kwa
mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Simbachawene
ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la
nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Chemba Juma Nkamia kuhusu Wakuu wa Wilaya
na Mikoa kuwa wababe katika maeneo yao ya kazi.
“Wakuu
wa Mikoa na Wilaya wanasimamia maeneo yao kwa mujibu wa sheria na wana
haki ya kuwachukulia hatua watumishi ambao hawatekelezi majukumu
waliyopewa,” alifafanua Simbachawene.
Aliendelea
kwa kusema kuwa, hata kama kuna Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni
wababe katika maeneo yao ya kazi hauwezi kusema kila Mkuu wa Mkoa au
Wilaya aliyechukua hatua dhidi ya mtumishi ambaye hawajibiki katika kazi
yake ni mbabe au muonevu.
Aidha,
Simbachawene amesema kuwa ni wakati sasa wa watumishi wa Umma
kutekeleza wajibu wao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. Kwani hakuna
kiongozi ambaye ataweza kumchulia hatua mtumishi ambaye anawajibika na
kazi zake kama alivyopangiwa.
Vile
vile amesema kuwa, wakuu hao wa Mikoa na Wilaya wamekuwa wakifanya kazi
nzuri katika maeneo wanayoyasimamia, kutokana na watumishi wengi wa
Serikali walikuwa wamejisahau kutekeleza wajibu wao na kufanya kazi
kimazoea.
No comments:
Post a Comment