Hakuna mtu asiyependa mafanikio katika kazi anayoifanya, mafanikio kwa
upande wa wachezaji wa kibongo ni kupata fursa ya kucheza soka la
kulipwa nje ya Tanzania hususan bara la Ulaya.
Watu wengi wamekuwa wakiwapigia kelele wachezaji wa Tanzania kupambana
kuhakikisha wanapata nafasi hizo wakiamini huko wataongeza uzoefu,
wataimarisha viwango vyao pamoja na weledi lakini pia hata vipato vyao
vitaongezeka.
Nilipopata fursa ya kuzungumza na Himid Mao Ninja au ‘Engine ya Boat’
sikuacha kumuuliza kama ana mpango wa kutoka Tanzania kwenda nje kucheza
soka nikiamini anaweza kutokana na uwezo wake mkubwa anaounesha akiwa
uwanjani kila anapoitumikia klabu yake ya Azam pamoja na timu ya taifa
ya Tanzania ‘Taifa Stars.
“Zimewahi kuja offer mbili, moja ilikuwa inatoka Slovenia na nyingine
ilikuwa inatoka Denmark sijui nini kilitokea lakini mwisho wa siku
hawakufikia makubaliano wao na Azam ila kwa upande wangu nilikuwa niko
tayari,” – Himid Mao
“Nilishaanza hadi michakato ya visa kwa ajili ya hilo deal la Denmark na
tulishalipa kila kitu lakini mwisho wa siku haikutoka ruhusa kutoka
Azam. Kipindi hicho tulikuwa kwenye mashindano ya Confederation
tunacheza mechi na Esparance kwa hiyo haikuwa rahisi kwa Azam kuniachia
kwa kipindi hicho.”
“Hakuna mtu asiyependa kucheza kwenye mazingira bora zaidi, lakini issue
ni kwamba mimi nipo kwenye mkataba kwa hiyo wao ndiyo wanashikilia haki
yangu mimi, wakisema nenda naenda, wakisema huwezi kwenda siwezi
kulazimisha kwa sababu wao ndio waajiri wangu wa sasa lakini ningekuwa
huru ningekuwa naamua kile nachotaka.”
No comments:
Post a Comment